Captain wa timu ya Hurunani kutoka Burundi akiwa amenyanyua kombe la Club Bingwa kanda ya Tano juu baada ya kulitetea kwa mara ya pili mara ya kwanza ilikuwa mwaka jana katika mashindano kama hayo yaliyo fanyika katika ardhi ya Burundi na kufanya Club hiyo sasa kuchukua Kikombe hicho mara tatu ndani ya Miaka Minne .
Naodha wa timu ya Wanawake ya USIU kutoka nchini Kenya akiwa ameshikilia Kikombe cha Ubingwa wa Club Bingwa kwa Wanawake kanda ya tano Mashindano yaliyomalizika hivi karibuni huko Kenya katika Jiji la Mombasa na kushuhudiwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho na Rais wa FIBA kanda ya Tano Hisham Hariri
Washindi wa tatu kwa Wanawake KCCA kutoka Kampala Uganda wakivishwa Medali na Maafisa wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mombasa (CBA)Madam Leila Ibrahim Awale katika Fainali za Club Bingwa Kanda ya Tano zilizo malizika Mombasa hivi karibuni.
Kamishna wa FIBA Camillo Ussene akimkabidhi zawadi ya mchezaji bora wa mashindano (MVP) mchezaji wa USIU Sarah Chan katika fainali iliyomalizika kwa USIU kuwafunga club ya KPA ya Mombasa huku Rais mpya wa kanda ya Tano Hisham Hariri akifuatilia tukuo hilo aliyevaa suti nyeusi.
Mwenyekiti wa Mpira wa Kikapu Mombasa Hilmi Ali kushoto akiongea jambo na Gavana wa Mombasa Hassan Joho muda mfupi baada ya Fainali ya Club Bingwa kanda ya tano kumalizika katika Jiji la Mombasa nchini Kenya huku Madam Leila Ibrahim akifuatilia maongezi kwa makini sana.