Monday, December 16, 2013

Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu Bara kuanza maandalizi ya Mashindano ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar yanayo tarajiwa kuanza mapema Januari

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wanahabari,

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania kupitia Kamisheni yake ya Waalimu, imefanya uteuzi wa Makocha wa timu ya Taifa itakayo kwenda kushiriki Michuano ya Maadhimisho ya Miaka 50 Mapinduzi ya Zanzibar ,Makocha hao ni Evarist Mapunda  anayefundisha timu ya Pazi akisaidiwa na Mohamed Mbwana anayefundisha Chon’gombe United.

Pamoja na Uteuzi huo ambao tayari umeanza kazi  umesha teua wachezaji watakao unda timu hiyo ambayo itaanza rasmi mazoezi tarehe 16 Desemba 2013 siku ya Jumatatu saa 10:00 Jioni katika Viwanja vya Don Bosco Upanga.

Jumla ya Wachezaji 18 walio chaguliwa kuunda timu hiyo pamoja na Vilabu wanavyo toka ni pamoja na .

Center:
1.Fadhili Abdallah  Lasser Hill Nairobi 
2.Arnod Tarimo    Bandari Tanga       
3.Sebastian Marwa  Pazi 
Forward:              
4.Moses Jackson  Mwanza 
5.Mwalimu Heri    JKT 
6.Lusajo Samwel  Oilers 
7.Denis Chibula    Pazi
Small Forward:
8.Salim Mchemba    ABC 
9.Enriko Agostino  Lord Barden
Shooting Guards:
10.Francis Mlewa  JKT 

11.Stefano Mshana  Jogoo 
12.Arron Salingo  Jogoo 
13.Sihaba Saidi  Lord Baden
Points Guards:
14.Mwaipungu Filbert ABC 

15.Allen Athumani  Tanga United
16.Evans Davis  Magoney 
17.Mussa Chacha  Magoney 
18.Baraka Sadiki  JKT      

TBF inawataka wachezaji wote waliochaguliwa kufika katika mazoezi siku ya jumatatu kama ilivyo agizwa na Makocha wa Timu hiyo wakiwa katika hali ya kuanza mazoezi.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wadau kutusaidia katika maandalizi ya timu hii katika kipindi chote cha Mazoezi kuanzia tarehe 16 Desemba 2013 hadi tarehe 07 Januari 2014 ambapo baada ya hapo timu itaondoka kuelekea Zanzibar tayari kwa Mashindano.

Shirikisho pia linapenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha wale wenye nia ya kuchukua fomu za Uongozi wa nafasi mbalimbali ndani ya Shirikisho sasa tumesogeza mbele hadi tarehe 20/12/2013 saa nane na nusu,hapo hawali tarehe ya mwisho ilikuwa ni tarehe 13/12/2013 lakini wadau wameomba tuongeze kwa wiki moja ili tuweze kupata idadi kubwa ya wagombe katika nafasi mbalimbali.  

Tunaendelea kuwaomba ndugu zetu wanahabari tuendelee kushirikiana katika kulipeleka mbele gurudumu la Maendeleo la Mpira wa Kikapu hasa katika kipindi hiki ambacho tunaingia katika chakato wa Uchaguzi Mkuu wa TBF ili tuweze kupata Viongozi Bora na watakao weza kufanya kazi kwa umakini mkubwa zaidi

No comments:

Post a Comment