Stephen Curry akiwa katika Clinic akiwaonyesha vijana waliofika katika mafunzo hayo namna ya kudunda mpira huku ukitizama mbele jumla ya vijana 100 walipata kushiriki mafunzo hayo.
Mchezaji wa Golden State Warriors ambaye ni balozi wa Malaria akigawa vyandarua kwa mmoja wa watoto waliopata nafasi ya kushiriki katika mafunzo ya siku moja yenye ujumbe wa kupiga vita ugonjwa wa Malaria 'Nothing But Net,pembeni yake ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Bwana Phares Magesa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay.
Mchezaji wa Golden State Warriors Stephen Curry akizungumza na watoto waliofika katika mafunzo ya Kupiga Vita ugonjwa wa Malaria wenye ujumbe " Nothing But Net "chini ya United Nations Foundation,mbeni yake ni Mchezaji wa ligi ya NBA timu ya Oklahoma City Thunder Mtanzania Hasheem Thabeeth.
Vijana 100 kutoka katika Shule Mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza mafunzo ya Mpira wa kikapu yenye ujumbe wa kupiga vita ugonjwa wa Malaria uliobeba unaosema Nothing But net katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay chini ya Balozi wa Malaria Stephen Curry mchezaji wa Golden State Warriors katika ligi ya NBA nchini Marekani.
Stephen Curry akiweka Saini kwenye Mipira, kama sehemu ya kumbukumbu mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay kwa ajili ya Mafunzo ya siku moja yenye kupiga Vita ugonjwa wa malaria, uliobeba ujumbe mzito wa Nothing But Net.
No comments:
Post a Comment