Saturday, August 24, 2013

Michuano ya Dume Cup imeingia katika siku ya pili baada ya Jumamosi kuchezwa michezo miwili kati ya Oilers Vs Chui na Pazi Vs chang'ombe United,matokeo ya michezo hiyo fuatilia hapo chini pamoja na michezo ya siku ya jumapili.

                                     INTER CLUB DUME CUP
                        23rd August To 01st Sept 2013 - DAR ES SALAAM
DATE
G.NO
TIME
TEAMS Vs TEAMS
                    
GRP
Q1
Q2
Q3
Q4
FINAL
25/08/2013
05
04 :00PM
JOGOO
PAZI
B
SUNDAY
06
06 :00PM
VIJANA
OILERS
A












Mchezaji wa Chui Daudi Machanya akipiga Danki katika Mashindano ya Dume Cup walipokuwa wakicheza na Oilers katika Viwanja vya Zanaki Upanga,katika mchezo huo Oilers alishinda kwa points79/78.
                                     INTER CLUB DUME CUP
                        23rd August To 01st Sept 2013 - DAR ES SALAAM
DATE
G.NO
TIME
TEAMS Vs TEAMS
                    
GRP
Q1
Q2
Q3
Q4
FINAL
24/08/2013
03
04 :00PM
OILERS
CHUI
A
 18/13
 20/30
 12/15
29/20
 79/78
SATURDAY
04
06 :00PM
PAZI
CHAN’G U
B
 10/14
16/09
15/13
12/12
53/48












       Wafungaji kwa Oilers:                                                         Wafungaji kwa Chui:
       Mussa Chacha PTS 24                                                           Barton Willy –PTS 14
       Amos Mgwasa PTS 22                                                          Daudi Machanya-PTS 26

       Wafungaji kwa Pazi :                                                     Wafungaji Chang’ombe United:
        Steve mtemihonda –PTS 19                                                 Godfrey Mlaliga –PTS 19
        Cray Bonny – PTS 11                                                          Adam Jigame – PTS 13

Mchezaji wa OILERS Dominic Zakharia(ganetti) akijaribu kufanya Shooting kwenye goli la Chui ,katika mchezo wao wa kwanza kwenye Viwanja vya  Shule ya Zanaki,Oilers alishinda katika mchezo huo kwa Poits 79/78.

Wachezaji wa timu ya Oilers yenye makazi yake Mikocheni Jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wake dhidi ya Chui katika Viwanja vya Zanaki Upanga,katika Michuano ya Dume Cup katika mchezo huo Oilersilishinda ndani ya sekunde tano ikiwa nyuma  kwa point 2 huku Chui wakiwa na point 78,Mchezaji Lusajo Samwel wa Oilers alipata mitupo huru na kubahatika kupata moja na kufikisha Point 77,Chui walijikuta wakifanya uzembe ambao ulipelekea kupokonywa mpira na Oilers na kufunga point 2 ambazo ziliwafanya waongoze kwa nusu kikapu yani 79/78 na mchezo kumalizika.


Wachezaji wa timu ya Chui yenye makazi yake Mwenge Jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wake dhidi ya Oilers katika Viwanja vya Zanaki,katika Michuano ya Dume Cup katika mchezo huo Chui alifungwa ndani ya sekunde tano akiwa anaongoza kwa point 78 huku Oilers wakiwa na point 76,Mchezaji Lusajo Samwel wa Oilers alipata mitupo huru na kubahatika kupata moja na kufikisha Point 77,Chui walijikuta wakifanya uzembe ambao ulipelekea kupokonywa mpira na Oilers kufunga point 2 ambazo ziliwafanya waongoze kwa nusu kikapu yani 79/78 na mchezo kumalizika.

No comments:

Post a Comment