Thursday, October 23, 2014

Shirika la Nyumba la Taifa hivi karibuni ilizindua Uwanja wa Mpira wa Kikapu katika eneo la Ilala Boma,uwanja unaokadiriwa kugharimu takribani Milioni 28, Ujenzi wa Uwanja huu ni moja ya Mikakati ya Shirika la Nyumba la Taifa kuboresha nyumba wanazo miliki, na kuwafanya wapangaji wake kuishi katika mazingira bora na salama,uwanja huu utawasaidia Vijana wa Ilala Flats na wale wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja huo kuweza kuutumia bila kwenda umbali mrefu kupata mafunzo ya Mpira wa Kikapu.

Mkurugenzi wa Programu Michael Maluwe kutoka Kampuni ya Grassroots Sports and Events kushoto akimkabidhi Cheti cha Shukurani Meneja Huduma kwa Jamii kutoka NHC Muungano Saguya Huku mmoja wa maofisa wa NHC Bi. Evarista Malya akishuhudia tukio hilo katika hafla ya ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu  Ilala mapema wiki iliyopita
Baadhi ya Vijana kutoka katika Shule za Jitegeme, Lord Baden Powell ya Bagamoyo pamoja na timu ya Ilala Flats ambao walioshiriki katika Ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu Ilala  Boma yalipo Mkazi ya watu wanaoishi katika Nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) wakiwa katika mafunzo ya siku moja ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo 

Baadhi ya Vijana kutoka katika Shule za Jitegeme, Lord Baden Powell ya Bagamoyo pamoja na timu ya Ilala Flats ambao walioshiriki katika Ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu Ilala  Boma yalipo Mkazi ya watu wanaoishi katika Nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) wakiwa katika mafunzo ya siku moja ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo 
Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania kwa Wanaume Evarist Mapunda ambaye pia ni kocha wa timu ya Pazi akiwa katika darasa la Mafunzo kwa Vijana walioshiriki uzinduzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu Ilala Boma hafla hiyo ilipambwa na shule ya Lord Baden Powell ya Bagamoyo,Jitegemee Secondary School pamoja na watoto wanaoishi katika Flats hizo za Ilala.
Julius Charles  mwenye umri wa mika 19 mchezaji wa shule ya lord Baden Powell akiwa na urefu wa 7.3  anasoma kidato cha tatu akiwa na Baadhi ya Vijana kutoka katika Shule za Jitegeme, Lord Baden Powell ya Bagamoyo pamoja na timu ya Ilala Flats ambao walioshiriki katika Ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu Ilala  Boma yalipo Mkazi ya watu wanaoishi katika Nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) wakiwa katika mafunzo ya siku moja ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo 
Naodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Lusajo Samwel akimsaidia kocha Evarist Mapunda kocha wa Timu ya Taifa wakitoa Mafunzo kwa watoto wanaoishi katika Flats za Ilala katika hafla ya uzinduzi wa Uwanja  wa Mpira wa Kikapu vijana hao wanafundishwa na Liana Mbaga katika siku za kawaida 
Katika Uzinduzi wa Uwanja huu pia Wasichana walishiriki vilivyo kupata mafunzo ya mpira wa Kikapu hawa ni baadhi ya wachezaji kutoka katika Shule za Jitegemee na Lord Baden powell

Maafisa wa NHC wakiwa na wakazi wa Ilala Flats pamoja na watoto wanaoishi katika Makazi hayo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Meneya wa NHC kanda ya Ilala kufungua rasmi  uwanja wa Mpira wa Kikapu uliojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa. 
 Maafisa wa NHC wakiwa na wakazi wa Ilala Flats pamoja na wanafunzi wa Jitegemee,lord Baden powell wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Meneya wa NHC kanda ya Ilala kufungua rasmi  uwanja wa Mpira wa Kikapu uliojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa .

 Meneja wa NHC Tawi la Ilala Jackson Maagi akimkabidhi mwakilishi wa Familia za Wapangaji wa NHC Ilala Mzee Alpius Machagge Jezi seti moja na Mpira mmoja kwa Niaba ya Mbunge wa jimbo la Ilala Mh.Mussa Hassan Zungu kwa ajili ya kuunga Mkono Michezo katika Jimbo lake, katika Tamasha la Ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu, Uliofanyika siku ya jumamosi tarehe 18/10/2014 Tamasha hilo lilifanyika katika  uwanja huo uliopo Ilala Boma yalipo Makazi ya wapangaji wa NHC na Kuratibiwa na Taasisi ya Michezo ya Grassroots Sports and Events.
  Mwakilishi wa Familia za wapangaji wa Shirika la Nyumba eneo la Ilala Boma Mzee Alpius Machagge akitoa neno la shukurani kwa Shirika la Nyumba katika Tamasha la Ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu, Uliofanyika siku ya jumamosi tarehe 18/10/2014 Tamasha hilo lilifanyika katika uwanja huo uliopo  Ilala Boma yalipo Makazi ya wapangaji wa NHC na Kuratibiwa na Taasisi ya Michezo ya Grassroots Sports and Events.
Meneja wa NHC kanda ya Ilala Jackoson Maagi akiongea na Vijana pamoja na wakazi wa Ilala Magorofani katika Tamasha la Ufunguzi wa Uwanja wa mpira wa Kikapu Uliofanyika siku ya jumamosi tarehe 18/10/2014 Tamasha hilo lilifanyika katika uwanja huo yalipo Makazi ya wapangaji wa NHC na Kuratibiwa na Taasisi ya Michezo ya Grassroots Sports and Events.
Liana Mbaga aka (Jigga) akiwa na Giovan Makassy aka.(Nguvu) wakiwa wanashauriana jambo kabla ya mchezo kati ya Ilala Flats na Lord Baden Powell haujaanza ikiwa ni moja ya sehemu ya Hafla ya Ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu Ilala.


Vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa kutoka Ilala Magorofani wakiwa katika Hafla ya Ufunguzi wa Uwanja wa Mpira wa Kikapu wakiongozwa na Mkurugenzi wa White Corner Pub Francis Cassidy (Chichi),Amosa Gelege (Banga), kheri kheri (Mpemba) Cristopher Leonard (Trigga the MC) na Omary Lyimo.