Monday, September 2, 2013

Matuklio ya Mchezo wa fainali kati ya OILERS VS JKT kutafuta Bingwa wa DUME fuatilia mtiririko wa picha na matokeo,nafasi ya tatu ilishikwa na jogoo ambaye alipata Kikombe, cheti na fedha Taslim Tsh 200,000 wakati JKT wakiambulia Tsh 300,000 cheti pamoja na Kikombe,pia timu zote shiriki walipata Vyeti vya Ushiriki


Wachezaji wa Oilers wakiwa katika Picha ya Pamoja na Meneja Masoko wa T Marc Bi.Lillian Silingi  ambao ndio wadhamini wa Michuano ya Dume Cup kupitia bidhaa yao ya Dume Condom pamoja na Katibu Mkuu Msaidizi wa TBF Mr.Michael Maluwe kulia na Makamu wa Rais wa BD Richard Jules, mara baada ya Mchezo wa fainali kati ya Oilers na JKT  kumalizika.

 Lusajo Samweli MVP wa Dume Cup Inter Club Basketball Tournament ambaye ni naodha wa timu ya Oilers akipokea kikombe pamoja na fedha taslim kiasi cha Tsh 500,000 kama zawadi ya ushindi baada ya kuilaza timu ya JKT kwa Points 78/69.



Mchezaji wa JKT mwenyejezi namba 11 akijaribu kumpiga Block mchezaji wa Oilers Musa Chacha katika mchezo wa Fainali ya Dume Cup uliomalizika hapo jana katika Viwanja vya Zanaki,Oilers walishinda kwa points 78/69.
Mchezaji wa Oilers Okare Emesu akijaribu kufuata rebound kwenye goli la JKT huku akiwa amezuiliwa na mkumbo Mgendi (Box Out) katika Fainali za kutafuta Dume kamili wa Mpira wa kikapu,Oilers alishinda kwa points 78/69 dhidi ya JKT.


Mchezaji wa JKT himid Choka akienda kufunga katika goli la Oilers mchezo uliojaa na msisimko na ushindani baada ya mikiki miki ya siku tisa za katika hatua za makundi na best of three katika hatua ya nusu fainali JKT alilala kwa oilers kwa points 78/69.



No comments:

Post a Comment