Msiba Mzito kwa familia ya Mpira wa Kikapu baada ya kumpoteza mmoja wa Viongozi waasisi wa kikapu Mkoa wa Morogoro Mosese Luoga aliyevaa kofia na Tshirt ya blue akiwa na timu ya Mzinga Corporation katika mashindano ya Muungano yaliyo fanyika Zanzibar 2010.
Luoga ambaye alishawahi kuwa Katibu wa Basketball Mkoa wa Morogoro kwa muda mrefu lakini pia Kocha wa Mpira wa Kikapu ambaye amezalisha wachezaji wengi Mkoani Morogoro.
Kikaputz imepokea taarifa kwa mmoja wa Makocha wa Mzinga na taarifa kamili atatupatia mara baada ya kujua taratibu na mipango kutoka katika familia ya Marehemu.
No comments:
Post a Comment