Friday, August 22, 2014

Baadhi ya Matukia yaliyo jiri katika siku ya Vijana Duniani katika maadhimisho yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu Jijini Dar es salaam.


Washindi wa Kwanza kwa Upande wa Wanaume Shule ya Secondari Lord Baden Powell ya Bagamoyo wakiwa katika picha ya Pamoja na Maafisa wa UNFPA na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Vijana  ambayo ipo chini ya  Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani .
Washindi wa Kwanza kwa Upande wa Wanawake timu ya DB Lioness wakiwa katika picha ya Pamoja na Maafisa wa UNFPA na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Vijana  ambayo ipo chini ya  Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani .

Mchezaji wa Timu ya Kizuka kutoka Morogoro akienda juu kwa ajili ya kufunga katika mchezo wa Tamasha la Vijana lililofanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam walipokutana na timu ya Segerea kutoka Tabata.
Mchezaji wa DB Lioness Rehema Silomba akijaribu kumzuhia mchezaji wa Magereza Queens katika Tamasha la Vijana lililofanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam timu ya DB Lioness walishinda Michezo miwili kati ya mitatu waliyotakiwa kucheza na kuwa Mabingwa.
 Mchezaji wa Timu ya Segerea Akijaribu kuchukua Rebond katika mchezo waliocheza dhidi ya Eagle ya Mbezi Beach katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani ambalo liliadhimishwa katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam.

Mchezaji wa Timu  ya Lord Baden Powell ya Bagamoyo akijaribu kumpita Mchezaji wa Shule ya  Makongo  katika mchezo waliocheza  hivi karibuni  katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani ambalo liliadhimishwa katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam

Mchezaji wa Timu  ya Segerea akienda lay -up na kufunga point mbili mbili muhimu kwa timu yake dhidi ya Eagle kutoka Mbezi Beach katika mchezo waliocheza  hivi karibuni  katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani ambalo liliadhimishwa katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam.


Sunday, August 17, 2014

Tamasha la Siku ya Vijana Duniani limefana kwa staili ya aina yake katika Viwanja vya chuo kikuu Jijini Dar essalaam,kwa timu mbalimbali za Mpira wa Kikapu kupamba Tamasha hilo ambalo lilikuwa na msisimko wa haina yake,pamoja na Mpira wa kikapu ambao ulishirikisha timu za secondari kama Lord Baden Powell ya Bagamoyo ,Makongo, na Kizuka kutoka Morogoro, pia kwa Wanawake timu ya DB Lioness na Magereza Queens walichuana vikali, huku Vilabu vipya katika medani ya kikapu Segerea Basketball Club na Eagle Basketball club pia viliwakilisha ipasavyo, mbali na kikapu pia Vijana mbalimbali washindanda katika Sanaa ya kuchora, na huduma Muhimu kuhusu Vijana zilitolewa na wadau kama vile Amref,Umati,Marie Stopes,TAA Net na UNFPA wakiwa kama waratibu wakuu kwa ushirikiano Mkubwa na kampuni ya GRASSROOTS SPORTS AND EVENTS.



  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani UNFPA Dkt. Natalia Kanem akiongea na Vijana katika maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa iliyo adhimishwa tarehe 16/08/2014 katika Viwanja vya Chuo Kikuu Dar es salaam ambapo wanamichezo wa Mpira wa kikapu walifana katika Tamasha hilo lililo beba ujumbe wa Afya ya Akili ni Muhimu (Mental Health Matters)
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana Mama Venerose Mtenga akiongea na Vijana ambao ni wanamichezo wa Mpira wa Kikapu waliokuwa wakiadhimisha siku ya Vijana Duniani katika Viwanja vya Chuo kikuu Jijini Dar es salaam tarehe 16/08/2014 Tamasha hilo lili bamba kwa timu mbalimbali kuonyesha uwezo wao.


 Wachezaji wa timu mbalimbali wakiwa wanasikiliza hotuba kutoka kwa viongozi wa UNFPA na Wizara ya Habari vijana Utamaduni na Michezo wakiwa tayari kuanza Tamasha hilo la aina yake  katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Vijana Venerose Mtenga akifunga point mbili kuashiria kuanza kwa Tamasha hilo la Vijana ambalo lilifana kuliko maelezo huku kila timu ikijitoa katika kuadhimisha siku hiyo kwa burudani ya Michezo na Sanaa ya uchoraji.
 Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Segerea yenye maskani yake Tabata Segerea jijini Dar es salaam ni moja ya timu mpya iliyosajiliwa kwa ajili ya kushiriki ligi ya mkoa wa Dar  salaam.


 Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Shule ya Secondari ya lord Baden Powell kutoka Mkoa wa Pwani Bagamoyo ni moja ya timu iliyoshiriki katika Tamasha hilo na kuibuka na medali ya dhahabu kama mshindi.


 Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Shule ya Secondari ya Kizuka kutoka Mkoa wa Morogoro ni moja ya timu iliyoshiriki katika Tamasha hilo.
                 
                         
Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Eagle yenye maskani yake Mbezi beach jijini Dar es salaam ni moja ya timu mpya iliyosajiliwa kwa ajili ya kushiriki ligi ya mkoa wa Dar  salaam.

Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya DB Lioness yenye maskani yake Upanga  jijini Dar es salaam ni moja ya timu kongwe za Wanawake na ni timu inayotarajiwa kwenda Nchini Kenya kwenye Jiji la Mombasa kwa jili ya Mashindano ya Zone V.

Thursday, August 14, 2014

Tamasha la Kuadhimisha siku ya Vijana Duniani yenye kauli mbiu Afya ya Akili ni muhimu (Mental Health Matters) linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Chuo kikuu Dar es salaam, siku ya Jumamosi tarehe 16 August 2013,kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, Timu mbalimbali zitashindana katika kuadhimisha siku hiyo, Tamasha hilo linaratibiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa,fuatilia ratiba ya michezo hapo chini...





        TAMASHA LA AFYA YA AKILI (MENTAL HEALTH) 16TH AUGOST 2014
             RATIBA YA MPIRA WA KIKAPU – UDSM COMPLEX

NO
KUNDI A – WANAUME(MEN)
KUNDI B WANAWAKE(LADIES)
1
MAKONGO HIGH SCHOOL
DONBOSCO LIONESS
2
BADEN/P HIGH SCHOOL
TANZANIA PRISONS QUEENS
3
KIZUKA SEKONDARI SCHOOL

4
SEGEREA BASKETBALL CLUB

5
EAGLES BASKETBALL CLUB


 TIME
GAME
NAME OF TEAM’S
GENDER
WINNER
09:00HRS.
01
KIZUKA SEC VS MAKONGO HIGH/SCH
MEN

09:40HRS.
02
DONBOSCO/L VS TANZANIA/P
LADIES

09:50HRS.
03
EAGLES VS SEGEREA
MEN

10:30HRS.
04
BADEN/P VS MAKONGO HIGH/SCH
MEN

10:50HRS.
05
KIZUKA/SEC VS SEGEREA
MEN

11:30HRS.
06
EAGLES VS BADEN/P
MEN

11:40HRS.
07
TANZANIA PRISONS VS DB LIONESS
LADIES

12:10HRS.
08
MAKONGO VS SEGEREA
MEN

12:40HRS.
09
KIZUKA VS EAGLES
MEN

13:30HRS.

LUNCH BREAK FOR ALL


14:30HRS.
10
SEGEREA VS BADEN/P
MEN

15:10HRS.
11
DONBOSCO/L VS TZ PRISONS QUEENS
LADIES

15:50HRS.
12
MAKONGO HIGH/SCHL VS EAGLES
MEN

16:30:HRS.
13
KIZUKA/SEC/SCHL VS BADEN/P
MEN



END OF BONANZA









Monday, December 16, 2013

Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu Bara kuanza maandalizi ya Mashindano ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar yanayo tarajiwa kuanza mapema Januari

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wanahabari,

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania kupitia Kamisheni yake ya Waalimu, imefanya uteuzi wa Makocha wa timu ya Taifa itakayo kwenda kushiriki Michuano ya Maadhimisho ya Miaka 50 Mapinduzi ya Zanzibar ,Makocha hao ni Evarist Mapunda  anayefundisha timu ya Pazi akisaidiwa na Mohamed Mbwana anayefundisha Chon’gombe United.

Pamoja na Uteuzi huo ambao tayari umeanza kazi  umesha teua wachezaji watakao unda timu hiyo ambayo itaanza rasmi mazoezi tarehe 16 Desemba 2013 siku ya Jumatatu saa 10:00 Jioni katika Viwanja vya Don Bosco Upanga.

Jumla ya Wachezaji 18 walio chaguliwa kuunda timu hiyo pamoja na Vilabu wanavyo toka ni pamoja na .

Center:
1.Fadhili Abdallah  Lasser Hill Nairobi 
2.Arnod Tarimo    Bandari Tanga       
3.Sebastian Marwa  Pazi 
Forward:              
4.Moses Jackson  Mwanza 
5.Mwalimu Heri    JKT 
6.Lusajo Samwel  Oilers 
7.Denis Chibula    Pazi
Small Forward:
8.Salim Mchemba    ABC 
9.Enriko Agostino  Lord Barden
Shooting Guards:
10.Francis Mlewa  JKT 

11.Stefano Mshana  Jogoo 
12.Arron Salingo  Jogoo 
13.Sihaba Saidi  Lord Baden
Points Guards:
14.Mwaipungu Filbert ABC 

15.Allen Athumani  Tanga United
16.Evans Davis  Magoney 
17.Mussa Chacha  Magoney 
18.Baraka Sadiki  JKT      

TBF inawataka wachezaji wote waliochaguliwa kufika katika mazoezi siku ya jumatatu kama ilivyo agizwa na Makocha wa Timu hiyo wakiwa katika hali ya kuanza mazoezi.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wadau kutusaidia katika maandalizi ya timu hii katika kipindi chote cha Mazoezi kuanzia tarehe 16 Desemba 2013 hadi tarehe 07 Januari 2014 ambapo baada ya hapo timu itaondoka kuelekea Zanzibar tayari kwa Mashindano.

Shirikisho pia linapenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha wale wenye nia ya kuchukua fomu za Uongozi wa nafasi mbalimbali ndani ya Shirikisho sasa tumesogeza mbele hadi tarehe 20/12/2013 saa nane na nusu,hapo hawali tarehe ya mwisho ilikuwa ni tarehe 13/12/2013 lakini wadau wameomba tuongeze kwa wiki moja ili tuweze kupata idadi kubwa ya wagombe katika nafasi mbalimbali.  

Tunaendelea kuwaomba ndugu zetu wanahabari tuendelee kushirikiana katika kulipeleka mbele gurudumu la Maendeleo la Mpira wa Kikapu hasa katika kipindi hiki ambacho tunaingia katika chakato wa Uchaguzi Mkuu wa TBF ili tuweze kupata Viongozi Bora na watakao weza kufanya kazi kwa umakini mkubwa zaidi

Tuesday, November 26, 2013

Rais wa TBF Mussa Mziya akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mustakabali wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania.

Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania leo limetangaza kuhairisha Mashindano ya Taifa Cup ambayo yalipangwa kufanyika Mkoani Mbeya kuanzia Decemba 30'2013 kutokana na Ukata wa fedha kwa ajili ya kuendesha Mashindano hayo.

Pamoja na Mashindano hayo ambayo yalipangwa kwenda sambamba na Vikao vya Bodi ya Shirikisho,Mkutano Mkuu na Uchaguzi wa  Shirikisho la Mpira wa Kikapu navyo vitakuwa vimeathirika na hivyo itapangwa tarehe nyingine na mahali pengine patakapo fanyika Vikao hivyo.

Soma Taarifa Kamili iliyotolewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania Mussa Mziya
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania akiongea na waandishi wa Habari leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Michezo la Taifa,akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa TBF ndugu Michael Maluwe.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu Wanahabari,

Kwa muda sasa kumekuwa na taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini na mchakato kuelekea uchaguzi mkuu wa Shirikisho. Leo tumeona ni vizuri tutolee ufafanuzi rasmi taarifa hizi.

Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini (TBF) napenda nichukue fursa hii leo kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya shughuli mbalimbali za Shirikisho na mchezo kwa ujumla kama ifuatavyo:

1.   Safari ya timu teule ya vijana kwenda Marekani
Wote tunafahamu kuwa Serikali ilikubali na kugharamia kumpata kocha wa kigeni wa mpira wa kikapu kuanzia Janauari mwaka huu. Kocha huyo Albert Sokaitis kutoka Marekani aliingia mkataba na TBF kwa niaba ya Serikali na kuanza rasmi kazi yake ya kufundisha na kuweka program mbalimbali za kuendeleza mchezo wa kikapu nchini.

Moja kati ya mambo aliyoyafanya Kocha katika program yake ilikuwa ni kuteua timu ya vijana, kuwanoa kwa muda na kisha vijana hao waende Marekani ambako wangepata mafunzo ya hali ya juu ya wiki 2. Gharama za safari hii ilikuwa zigharimiwe na TBF kwa upande wa nauli ya kwenda na kurudi na wadau wengine huko Marekani kwa upande wa vifaa, malazi, chakula na usafiri wa ndani, ambao kwa upande wao walisha andaa yote hayo.

Kwa bahati mbaya, wakati Kocha anapendekeza safari hii kwa vijana, bajeti kwa ajili ya kazi zake hapa kwa mujibu wa mkataba ilikwishatolewa na Serikali na hatukuwa na fungu lolote kwa ajili ya nauli kwa vijana hawa. Juhudi za TBF kupata fedha kwa ajili ya nauli kwa timu haikuzaa matunda mpaka tarehe ya safari. Hivyo tuliwasiliana na Kocha kuomba kuahirisha safari mpaka wakati tutakapopata fedha. Kocha ametupangia nafasi mwezi March 2014 kwa safari hiyo

TBF kwa sasa tunafanya juhudi kwa kushirikiana na mamlaka husika kuweza kupata fedha hizo na timu iweze kusafiri hapo mwezi March kama ilivyopangwa.

2.   Azma ya Kocha kujiuzulu

Kumekuwapo na taarifa pia kuwa Kocha Albert Sokaitis kujiuzulu kufanya kazi ya kufundisha na kuendeleza mpira wa kikapu Tanzania. Ni kweli Kocha alitoa tamko hilo la kujiuzulu, lakini hii ilitokana na kuvunjika moyo kwake kwa kushindwa kwetu kuwezesha vijana hawa kusafiri kama alivyopendekeza. Lakini kama nilivyosema awali kuwa jambo hili lilikuwa juu ya uwezo wetu kwa wakati ule kutokana na kuwa zilihitajika takriban Sh. Milioni 50 kwa ajili ya nauli zao, fedha ambazo TBF haikuwa nazo.

Hata hivyo, kwa kuwa suala hili la kuwepo kwa Kocha hapa ni la kimkataba zaidi, TBF kwa kushirikiana na mamlaka husika tulilifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo (kwa simu) na Kocha ili kupata ufumbuzi.

Baada ya mkutano huo na mawasiliano yaliyofuatia kikao hicho, tumekubaliana na Kocha kuwa ataendelea na kazi hii kama tulivyokubaliana awali. Tayari Kocha ameshawasilisha mapendekezo yake na program ya mwaka kwa uratibu na utekelezaji. Vilevile Kocha anaendelea kutuma vifaa mbalimbali ikiwemo mipira kwa ajili ya vijana wetu.

3.  Mashindano ya Taifa Cup 2013

Shirikisho lilipanga kufanya mashindano ya Taifa Cup mwaka huu jijini Mbeya baada ya mkoa wa Mbeya kuomba kuyaandaa nasi kukubali ombi lao. Yalipangwa kufanyika kuanzia tarehe 28/11/2013 mpaka 8/12/2013 na kufuatiwa na mikutano ya Shirikisho na Uchaguzi mkuu wa TBF.

Kwa bahati mbaya, kutokana na sababu zifuatazo, na baada ya mashauriano na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TBF, natangaza kwamba mashindano haya sasa yameahirishwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.

(i)           Ukosefu wa fedha za kutosheleza kuendeshea mashindano sambamba na mikutano na uchaguzi wa Shirikisho. Kwa uchache tulihitaji si chini ya Sh. Milioni 10.
(ii)          Wenyeji mkoa wa Mbeya kuomba kuyaahirisha kutokana na kutokamilika kwa wakati kwa viwanja vitakavyotumika kwa mashindano hayo.
(iii)        Mikoa michache kuthibitisha kwa maandishi ushiriki wao katika mashindano.

4.  Mkutano Mkuu na Uchaguzi Mkuu wa TBF

Ndugu Wanahabari, mwaka huu ni mwaka wa mwisho wa kipindi cha uongozi kwa viongozi wa TBF walio madarakani kwa sasa. Hivyo kuwajibika kuwa na uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho, sambamba na mikutano ya Bodi ya Shirikisho na Mkutano Mkuu wa wanachama wetu (vyama vya mikoa vilivyosajiliwa).

Mikutano yote hii na uchaguzi vilipangwa kufanyika sambamba na mashindano ya Taifa Cup yaliyokuwa yafanyike Mbeya kuanzia tarehe 28 Novemba mpaka 8 Desemba 2013. Kwa bahati mbaya tena, kutokana na kuahirishwa kwa mashindano ya Taifa cup, kumeathiri pia na kulazimika kuahirisha shughuli hizi za mikutano na uchaguzi huko Mbeya. Shughuli hizo sasa zitafanyika katika tarehe na mahali patapopangwa baadae na Kamati ya Utendaji ya TBF lakini ndani ya mwaka huu wa 2013. Shughuli za utoaji wa fomu kwa wagombea bado inaendelea na inaratibiwa na Baraza la MIchezo la Taifa (BMT). Hivyo wote wanaotarajia kugombea katika nafasi zilizotangazwa awali katika uchaguzi huo wanaombwa waendelee kuchukua fomu.

Imetolewa na
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)

Monday, October 21, 2013

New Orleans selected to host 2014 NBA All-Star Game

The 2014 All-Star Game will be played at New Orleans Arena, home of the Hornets, pending the completion of arena and hotel agreements. This will mark the second time that NBA All-Star will be hosted in New Orleans, having previously been held in the "Crescent City" in 2008.

"There is no better place to celebrate and showcase the NBA than in New Orleans, a city with a rich tradition of hosting major events that is second-to-none," said Stern. "Our 2008 NBA All-Star festivities proved a terrific experience for everyone involved, and we anticipate 2014 will be even better." A weeklong celebration, NBA All-Star showcases NBA players' passion for basketball, engagement with fans, commitment to community and respect for the history and tradition of the game.

The 2014 All-Star Game will mark the 30th year that Turner Sports will provide NBA All-Star coverage, and the 12th consecutive year the All-Star Game will be televised in primetime on TNT. The All-Star Game will be seen by a worldwide television audience in more than 200 countries and territories and in more than 40 languages.

No city in America has attracted such a string of major sporting events in such a short period of time. This proves that Louisiana continues to be a world class destination for major events. These events will generate millions in economic return for the city and state, provide thousands of jobs for our citizens and provide immeasurable national and international publicity for our great state.

Durant shows he's can carry Thunder alone


OKLAHOMA CITY -- When the team has a roster that's pretty much set, experience and a proven record of winning, the preseason is a chance to do some evaluating.

Kevin Durant is still good.
 

OK, no news there, but what Tuesday night against the Nuggets showed was Durant is good enough to carry a team, this Oklahoma City team, by himself.
 


And yes, he's gonna have to do it for a good portion of this season, so might as well get some run doing it now during the preseason.

In 22 minutes, Durant scored 36 points on 13-of-20 shooting. He had six rebounds and four assists and if Denver's Anthony Randolph tries to guard him in the regular season anything like he did Tuesday in Oklahoma City, Durant will score 80 points.

Durant didn't play after the 5:06 mark of the third quarter, and rightfully so. It's time to save his legs. If he doesn't play another minute of the exhibition schedule, that would be too much, and while he'd never admit it, this season is going to come down to how much Durant can do.

It's been a lot in the past half-decade, but in the playoffs last year against Memphis, it wasn't enough. Durant faltered in the last few minutes of the last four games and the Thunder lost them all. That's what happens when Russell Westbrook isn't available and no one else can be counted on with any real regularity.

So, yes, coach Scott Brooks is – he has to be, right? - using the preseason desperately trying to figure out who will play, what rotations and lineups to use and who will be the No. 2 to Durant.

And Durant does have help. Serge Ibaka and Reggie Jackson are good complements, but this preseason hasn't been the best for uncovering any truths about Jeremy Lamb or Steven Adams. Not yet, anyway.

We've seen Durant do it before and we saw it again Tuesday. And not to take too much from a preseason game, but once again Durant didn't have much consistent help. Durant made four-of-eight 3-pointers. The rest of the team went one-of-nine.


"We got better tonight," Brooks said, talking defense and team chemistry and all the kind of things coaches say because they believe them. But what about the shooting? What about the help for Durant?

"We're not pushing the panic button after three preseason games," Brooks said. "We have guys, I believe in their shooting ability. We're going to keep working on it."

And Durant will have to keep working, too. The question will be how many minutes and how much pressure he'll put on himself to carry the team.

Durant may not just be feeling the pressure to play for his teammates. He's going to have to score for them, too.