Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani UNFPA Dkt. Natalia Kanem akiongea na Vijana katika maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa iliyo adhimishwa tarehe 16/08/2014 katika Viwanja vya Chuo Kikuu Dar es salaam ambapo wanamichezo wa Mpira wa kikapu walifana katika Tamasha hilo lililo beba ujumbe wa Afya ya Akili ni Muhimu (Mental Health Matters)
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana Mama Venerose Mtenga akiongea na Vijana ambao ni wanamichezo wa Mpira wa Kikapu waliokuwa wakiadhimisha siku ya Vijana Duniani katika Viwanja vya Chuo kikuu Jijini Dar es salaam tarehe 16/08/2014 Tamasha hilo lili bamba kwa timu mbalimbali kuonyesha uwezo wao.
Wachezaji wa timu mbalimbali wakiwa wanasikiliza hotuba kutoka kwa viongozi wa UNFPA na Wizara ya Habari vijana Utamaduni na Michezo wakiwa tayari kuanza Tamasha hilo la aina yake katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Vijana Venerose Mtenga akifunga point mbili kuashiria kuanza kwa Tamasha hilo la Vijana ambalo lilifana kuliko maelezo huku kila timu ikijitoa katika kuadhimisha siku hiyo kwa burudani ya Michezo na Sanaa ya uchoraji.
Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Segerea yenye maskani yake Tabata Segerea jijini Dar es salaam ni moja ya timu mpya iliyosajiliwa kwa ajili ya kushiriki ligi ya mkoa wa Dar salaam.
Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Shule ya Secondari ya lord Baden Powell kutoka Mkoa wa Pwani Bagamoyo ni moja ya timu iliyoshiriki katika Tamasha hilo na kuibuka na medali ya dhahabu kama mshindi.
Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Shule ya Secondari ya Kizuka kutoka Mkoa wa Morogoro ni moja ya timu iliyoshiriki katika Tamasha hilo.
Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Eagle yenye maskani yake Mbezi beach jijini Dar es salaam ni moja ya timu mpya iliyosajiliwa kwa ajili ya kushiriki ligi ya mkoa wa Dar salaam.
Viongozi na Maafisa wa UNFPA na UNDP pamoja na Mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya DB Lioness yenye maskani yake Upanga jijini Dar es salaam ni moja ya timu kongwe za Wanawake na ni timu inayotarajiwa kwenda Nchini Kenya kwenye Jiji la Mombasa kwa jili ya Mashindano ya Zone V.
No comments:
Post a Comment