Washindi wa Kwanza kwa Upande wa Wanaume Shule ya Secondari Lord Baden Powell ya Bagamoyo wakiwa katika picha ya Pamoja na Maafisa wa UNFPA na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Vijana ambayo ipo chini ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani .
Washindi wa Kwanza kwa Upande wa Wanawake timu ya DB Lioness wakiwa katika picha ya Pamoja na Maafisa wa UNFPA na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Vijana ambayo ipo chini ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani .
Mchezaji wa Timu ya Kizuka kutoka Morogoro akienda juu kwa ajili ya kufunga katika mchezo wa Tamasha la Vijana lililofanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam walipokutana na timu ya Segerea kutoka Tabata.
Mchezaji wa DB Lioness Rehema Silomba akijaribu kumzuhia mchezaji wa Magereza Queens katika Tamasha la Vijana lililofanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam timu ya DB Lioness walishinda Michezo miwili kati ya mitatu waliyotakiwa kucheza na kuwa Mabingwa.Mchezaji wa Timu ya Segerea Akijaribu kuchukua Rebond katika mchezo waliocheza dhidi ya Eagle ya Mbezi Beach katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani ambalo liliadhimishwa katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa Timu ya Lord Baden Powell ya Bagamoyo akijaribu kumpita Mchezaji wa Shule ya Makongo katika mchezo waliocheza hivi karibuni katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani ambalo liliadhimishwa katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam
Mchezaji wa Timu ya Segerea akienda lay -up na kufunga point mbili mbili muhimu kwa timu yake dhidi ya Eagle kutoka Mbezi Beach katika mchezo waliocheza hivi karibuni katika Tamasha la siku ya Vijana Duniani ambalo liliadhimishwa katika Viwanja vya Chuo kikuu jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment