Tuesday, August 13, 2013
TBF yatangaza kufuta Clinic ya Hasheem Thabeeth kwa mwaka huu kutokana na Mchezaji huyo wa NBA kuitwa na Club yake kwenda kwenye Ratiba Maalum na baadaye ataudhuria Mafunzo ya Vijana wa Africa maarufu kama Basketball Without Border (BWB) nchini Afrika ya kusini
Clinic ya Hasheem Thabeeth ilipangwa ifanyike mwezi August kuanzia tarehe 16 - 18 katika Mkoa wa Arusha, na kushirikisha Vijana wasio pungua 200 kutoka katika Mikoa sita ya Bara na Visiwani ambayo, ni Dar es salaam, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro, Zanzibar,na wenyeji Arusha.
kutokana na mwingiliano wa Ratiba TBF imelazimika kufuta Clinic hiyo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa Hasheem juu ya Club yake ya Oklahoma City Thunder kumuitaji haraka kurudi nchini Marekani.
Hasheem Thabeeth baada ya Ratiba ya Club yake pia atakwenda Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuudhuria Mafunzo ya Vijana ambayo yanajulikana kama Basketball Without Border (BWB) program ambayo ipo chini ya NBA Africa na kuudhuriwa na wachezaji wa ligi ya NBA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment