Mchezaji wa Shule ya Lord Baden Powell akijaribu kupangua Defensi ya Shule ya Secondari Ape Rugunga Kutoka Rwanda ambapo katika mchezo huo timu hiyo ya Rwanda ilishinda kwa 48 -35 katika Michuano ya Feassa inayoendelea Jijini Dar es salaam katika Viwanja vya Taifa
Mchezaji wa Lord Baden powell akijaribu kuona namna ya kutoa pasi kwa mchezaji mwenzake wakati mchezaji wa timu ya Ape Rugunga akiwa makini kwenye defensi Lord Baden wanawake walipoteza mchezo huo.
Wachezaji wa Ape Rugunga kutoka Rwanda wakicheza Box out wakati wakisubiri Rebond katika mchezo wa kwanza wa Michuano ya Shule za Secondari Afrika Mashariki (FEASSA) inayoendelea katika Viwanja vya Taifa Jijini Dar es salaam Shule ya Ape waliibuka na Ushindindi wa pointi 48 - 35
Coach Roinnie Owino wa Kenya akiwa pamoja na Coach Evarist Mapunda wa Tanzania wakifuatilia Michuano ya Shule za Secondari Afrika Mashariki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambayo imeanza rasmi tarehe 24 August 2014 na kutarajiwa kumalizika tarehe 31 Aug 2014.Timu ya Shule ya Sekondari Tigoi kutoka nchini Kenya wakipewa maelekezo na kocha wao katika michezo inayoendelea ndani ya Viwanja vya Taifa jijini Dar es salaam timu hiyo ilipomenyana vilivyo na St Mary Kitende kutoka Uganda ambapo St Mary walishinda kwa 58- 28.
Mchezaji wa Timu ya Tigoi akijaribu kuwapita Defensi ya St.Mary Kitende katika Michuano ya Feassa inayoendelea katika Viwanja vya Taifa jijini Dar es salaam na kuudhuriwa na Mashabiki mbalimbali wa jiji la Dar es salaam michezo hiyo inatarajiwa kumalizika tarehe 31 Aug 2014
No comments:
Post a Comment