Coach Ronnie Owino wa anayefundisha shule ya secondari Upper Hill nchini Kenya akijaribu kutoa maelekezo kwa wachezaji wake nini wanapaswa kufanya wanapokuwa uwanja upande wa defensi timu hiyo ilishinda Pointi 74-49 dhidi ya ETS Kamenge.
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Wachezaji wa Timu ya Upper Hill na mchezaji wa ETS Kamenge wakigombe Rebound katika mchezo uliochezwa leo asubuhi katika viwanja vya Taifa Jijini Dar es salaam na timu ya Upper Hill kuibuka na Ushindi wa kutosha kabisa.
Mchezaji wa Upper Hill Joshua Omolo akifuata mpira Rebound ya offence wakati mchezaji wa timu ya ETS Kamenge akijaribu kumzibiti asifunge kikapu mchezo ulimalizika kwa timu ya Upper Hill kutoka kifua mbele kwa Pointi 74 - 49 katika michuano ya Shule za sekondari Afrika Mashariki inayoendelea Uwanja wa Taifa.
Martine Mugambi mchezaji wa Upper Hill akiwa na mpira na kutafuta mbinu mbadala wa kupata Kikapu muhimu kwa timu yake walipokuwa wakicheza na ETS Kamenge katika viwanja vya Taifa Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment