Kama mnavyo jua timu ya Vijana ni timu pekee ya Wanaume, ambayo mpaka sasa ipo kwenye nafasi nzuri ya kwenda kwenye Michuano ya Kanda ya Tano Afrika, itakayo fanyika Bunjumbura - Burundi kuanzia August 05 - August 11 2013.Baada ya timu za Jeshi ABC na Wanawake ya Jeshi Stars kujiondoa kushiriki Michuano hiyo mikubwa kwenye ukanda wetu.
Na kwa wale wanaojua ukubwa wa mashindano haya natumaini wanajua pia na gharama zake zilivyo hivyo basi popote pale ulipo support yako ni muhimu kwa Club ya Vijana.
Timu nyingine ambayo inategemea kwenda kwenye mashindano ni timu ya Wanawake ya Don Bosco Lioness ila Mpaka sasa bado haijatuma hata majina ya wachezaji kwa ajili ya kupata leseni za FIBA .
No comments:
Post a Comment